دانلود کتاب WESTMINSTER SHORTER CATECHISM IN SWAHILI (KATEKISIMU FUPI)
by Daniel J. Seni
|
عنوان فارسی: کاتشيزم WESTMINSTER SHORTER به زبان انگليسي (کاتکيزم کوتاه) |
دانلود کتاب
جزییات کتاب
Tumelazimika kutoa ufafanuzi mfupi ili kupinga majaribio ya wazushi ambao hulaghai washirika kwa madai kwamba Katekisimu iko kidini sana, na siyo kiroho, madai ambayo hayana ukweli wowote. Watumiaji wanapaswa kujua kwamba Katekisimu hii imesheheni mafundisho ya msingi ya Ukristo kwa kuzingatia Biblia Takatifu.
Kuna aina kuu mbili za Katekisimu za Westminister; Katekisimu fupi na Katekisimu ndefu. Katekismu fupi ina maswali 107 na Katekisimu ndefu ina maswali 196. Hii ni Katekisimu fupi ambayo ilianza kuandikwa mwaka 1646 na kumalizika mwaka 1647. Iliandaliwa na sinodi ya wanatheolojia Warefomati wa Uingereza na Scotland. Makanisa mengi ya “Ki-Refomati” (Reformed Churches), yakiwemo makanisa ya Ki-Presibiteriani hutumia Katekisimu hii.
Hivyo basi, dhima yetu ni kuhakikisha kwamba washirika wote wanafundishwa misingi ya imani ya Kikristo kwa kuzingatia Katekisimu hii. Na kwamba baada ya kumakinika katika Katekisimu fupi, pia wawe tayari kumakinika katika Katekisimu ndefu.
Tafsiri hii imetokana na toleo la Kiingereza cha Kisasa, na hivyo tumejaribu kuzingatia maneno-msingi na tahajia yake, na pia tumejaribu kwa umakini kuzingatia maana ya awali.
DANIEL JOHN SENI