دانلود کتاب EKKLESIOLOJIA: MAFUNDISHO YA KIKRISTO KUHUSU KANISA (MTAZAMO WA KIHISTORIA)
by Daniel J. Seni (Mwandishi)
|
عنوان فارسی: اکولوژی: دکترین مسیحی درباره کلیسا (دیدگاه تاریخی) |
دانلود کتاب
جزییات کتاب
"Ni mfululizo wa masomo katika uwanja wa Teolojia Pangilifu (systematic Theology). Katika kitabu hiki tunashughulikia mafundisho ya Kikristo kuhusu kanisa.
Hiki siyo kitabu cha Historia ya Kanisa, bali ni mafundisho kuhusu kanisa, yaani “eklezia.” Katika kitabu hiki nimefanya uchambuzi wa kanisa kwa kuzingatia mtazamo wa kibiblia, kihistoria, na kitamaduni. Hata hivyo, mahitimisho yote yamezingatia mtazamo wa Teolojia Iliyoboreshwa au Refomati (Reformed Theology), kwani ninaamini kwamba ndio mtazamo wa Kibiblia, ingawa ama kwa hakika hauwezi kukosa changamoto.
Ikumbukwe kwamba kanisa ni mojawapo ya taasisi ambayo inavutia watu wengi katika dunia hii. Na pengine, mojawapo ya sababu kuu ni kwamba kanisa lilianzishwa na Mungu mwenyewe kwa ajili ya kusudi lake maalumu. Katika muono huo, tunahitaji sasa kujua kanisa ni kitu gani, lilianzia wapi? Liliendeleaje na linaendeleaje? Kipi kinachoonesha kwamba hili ni kanisa? Zipi ni sifa anuwai za kanisa la kweli? Haya ni maswali machache ambayo yamejibiwa katika katika kitabu hiki."