دانلود کتاب SOTERIOLOJIA: MAFUNDISHO YA KIKRISTO KUHUSU WOKOVU
by Daniel J. Seni (Mwandishi)
|
عنوان فارسی: استریولوژی: دكترین مسیحی درباره نجات |
دانلود کتاب
جزییات کتاب
Huu ni mfululizo wa masomo katika uwanja wa “Teolojia Pangilifu” (Systematic Theology). Sasa tunashughulikia somo la Soteriolojia, yaani somo linalohusu “wokovu wa mwanadamu.”
Siku hizi pengine inaweza kudhaniwa kwamba kila Mkristo anajua maana ya wokovu na upatikanaji wake. Watumishi wengi wasiopenda kujishughulisha huishia kusema “Yesu anaokoa” bila kufafanua maana ya sentensi hii nyepesi na rahisi sana. Ni kweli katika muktadha wa misiolojia tunaweza kutumia sentensi nyepesi kama hizi bila kuzitolea ufafanuzi kwa sababu wale tunaowaambia tunachukulia kwamba hawajui kitu chochote.
Siku hizi kuna makanisa yanayojiita, “makanisa ya wokovu” ambayo hudai kuhubiri wokovu wa kweli. Hata hivyo, nimegundua mapungufu mengi katika mafundisho yao kuhusu wokovu kwa kudhania kwamba wokovu ni tukio la sekunde moja.
Ama kwa hakika, wokovu ni mchakato; ingawa yawezekana michakato hiyo isipangiliwe vizuri na kuleta maana, lakini bado tunapaswa kujua kwamba wokovu ni mchakato. Mchakato wa kumwokoa mwanadamu unaanzishwa na Mungu mwenyewe na kumaliziwa pia na Mungu mwenyewe.
Katika kitabu hiki, kwa namna ya upekee nimejaribu kufafanua kwa undani kuhusu michakato hiyo kwa kuzingatia ufafanuzi wa teolojia iliyoboreshwa (Reformed Theology)
Kitabu hiki si kwa wale ambao wameshazaja akili zao mafundisho mbalimbali ya wokovu, na hivyo hawataki kubadilisha mwelekeo na kujifunza upya. Pia kitabu hiki si kwa wazembe, wasiopenda kushughulisha akili zao. Si kwa wale wanaopenda kutafuniwa tu, bali ni kwa wale ambao wanaweza kuvunja mifupa na kuelewa.
Ninakutia moyo kwamba unaposoma kitabu hiki unahitaji kusoma katika hali ya utulivu, na kumwomba Roho Mtakatifu akusaidie ili uweze kuelewa zaidi na zaidi somo hili muhimu.
Marejeleo mengi yaliyotumika katika kitabu hiki yanatokana na lugha ya Kiingereza, hivyo basi, kwa wale ambao wana uwezo wa kusoma Lugha ya Kiingereza wanashauriwa kupata baadhi ya nakala za vitabu hivyo kwa sababu ni muhimu sana.
Yawezekana katika kitabu hiki ninaweza nisikubaliane na baadhi ya tafsiri ya kambi ya Teolojia Iliyoboreshwa kwa asilimia zote, lakini kwa kweli kwa sehemu kubwa inakubaliana na mafundisho halisi ya Neno la Mungu.